Yanga yarudi kwa Dala

Joel JJ By Joel JJ • 5th June 2026


Yanga yarudi kwa Dala

Yanga wamehuisha tena mpango wao wa kumsajili winga wa kimataifa wa Angola, Gelson Dala, kuelekea dirisha kubwa la usajili linalotarajiwa kufunguliwa mwezi ujao.

Katika dirisha dogo la usajili lililopita, Yanga ilifanya juhudi kubwa kumleta Dala kutoka klabu ya Qatar ya Al Wakrah SC, lakini mpango huo haukufanikiwa baada ya changamoto za uhamisho wake.

Kwa mujibu wa taarifa, Yanga ilikuwa imepanga kufanya usajili wa pamoja wa Dala na Laurindo Aurelio “Depu”, lakini ilifanikiwa kumsajili Depu pekee, huku Dala akibaki katika klabu yake ya Qatar.

Baada ya kushindikana kwa mpango huo, mabingwa hao wa Tanzania Bara waliendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili Buba Jammeh katika hatua za mwisho za dirisha dogo, usajili ambao ulipendekezwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pedro Goncalves.

Goncalves, kocha wa zamani wa Yanga, alikuwa ameweka wazi kuwataka wachezaji wote wawili, Dala na Depu, kutokana na uzoefu wake nao akiwa kwenye timu ya taifa ya Angola.

Sasa taarifa mpya zinaeleza kuwa Yanga bado haijakata tamaa, na mpango wa kumsajili Dala upo palepale, ambapo kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo katika dirisha lijalo la usajili.

Inaelezwa kuwa Yanga na Dala walikuwa tayari wamefikia makubaliano ya awali, lakini dili hilo lilikwama kutokana na klabu yake ya Al Wakrah kutokuwa tayari kumruhusu kuondoka wakati wa dirisha dogo.

Endapo mazungumzo yatakamilika kwa mafanikio, Dala anaweza kuwa moja ya usajili mkubwa kwa timu hiyo katika kujiandaa na msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.