Ederson kutua Manchester United

Joel JJ By Joel JJ • 3rd June 2026


Ederson kutua Manchester United

Kiungo wa Atlanta Ederson amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Manchester United katika dili linalofikia thamani ya takriban €45 milioni pamoja na nyongeza (add-ons).

Makubaliano kati ya klabu hizo mbili yamekamilika baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa wiki kadhaa, huku dili likifungwa rasmi na sasa kinachosubiriwa ni hatua za mwisho za kimatibabu (medical tests) na taratibu za usajili kabla ya tangazo rasmi kutolewa.

Usajili wa Kwanza wa Carrick

Inaripotiwa kuwa Éderson atakuwa usajili wa kwanza wa kocha mpya wa Manchester United, Michael Carrick, katika dirisha hili la majira ya joto, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuijenga upya timu hiyo kwa msimu ujao.

Carrick anaelezwa kuwa na mpango wa kuimarisha eneo la kiungo kwa kuongeza nguvu, uimara na ubunifu, na Éderson anaonekana kuwa chaguo sahihi kutokana na uwezo wake wa kukaba, kupandisha mashambulizi na kudhibiti tempo ya mchezo.

Vyanzo vya karibu na dili hilo vinasema kuwa mazungumzo kati ya Manchester United na Atalanta yalikuwa yameingia hatua za mwisho kwa muda, na sasa kila kitu kimekamilika kwa pande zote mbili. Mkataba wa miaka minne umekubaliwa kati ya mchezaji na klabu mpya.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.