Pacome, Zimbwe Jr waongeza nguvu Yanga

Joel JJ By Joel JJ • 2nd June 2026


Pacome, Zimbwe Jr waongeza nguvu Yanga

Klabu ya Yanga SC imepokea boost kubwa kuelekea mechi za mwisho wa msimu baada ya wachezaji wake muhimu, Pacome Zouzoua na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, kurejea kikosini na kuanza mazoezi kikamilifu.

Kiungo mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Pacôme Zouzoua, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliorejea mazoezini jana katika kituo cha KMC Complex, akianza tena maandalizi ya mechi zilizobaki baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeraha ya goti.

Pacome alipata majeraha hayo katika mchezo dhidi ya Singida Black Stars, hali iliyomfanya akose baadhi ya mechi muhimu kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA. Hata hivyo, sasa amerejea akiwa fiti na kushiriki kikamilifu katika program za mazoezi chini ya benchi la ufundi.

Urejeo wake unatajwa kuwa muhimu sana kwa Yanga SC, ambayo inaendelea kupambana kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kushiriki mechi ngumu za mashindano ya Kombe la CRDB.

Katika upande mwingine, beki wa kushoto wa Yanga, Mohamed Hussein Zimbwe Jr, naye amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha. Sasa ameonekana akiwa fiti na kushiriki mazoezi yote pamoja na wenzake.

Uwepo wa Zimbwe Jr unatoa nafuu kubwa kwa kikosi cha Yanga, hasa katika eneo la ulinzi wa pembeni, ambapo uzoefu wake unahitajika katika mechi muhimu zinazokuja.

Mazoezi ya Yanga yameendelea ambapo jana na leo wachezaji wamefanya session mbili tofauti. Asubuhi walipitia programu maalum ya mazoezi ya gym, kabla ya mchana kuendelea na mazoezi ya uwanjani chini ya makocha Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.