Majeraha yamuondoa Fei Toto kikosi cha Stars

Joel JJ By Joel JJ • 1st June 2026


Majeraha yamuondoa Fei Toto kikosi cha Stars

Kiungo mshambuliaji, Feisal Salum, amekosa nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, baada ya kugundulika kuwa na majeraha yaliyomfanya ashindwe kuendelea na majukumu ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Cliford Ndimbo, Fei Toto alifika kambini akiwa ameitwa kwenye kikosi hicho, lakini hali yake ya afya ilibainika kutokuwa sawa.

Ndimbo amesema baada ya mchezaji huyo kufanyiwa uchunguzi wa kina na jopo la madaktari, iligundulika kuwa hataweza kushiriki mechi mbili za kirafiki zilizo mbele ya timu hiyo.

“Baada ya Fei Toto kuwasili kambini alionekana hayuko fiti na alipofanyiwa uchunguzi zaidi jopo la matabibu limeona hatoweza kucheza mechi hizo mbili za kirafiki,” alieleza Ndimbo.

Pamoja na kuondoka kwa Fei Toto kwenye kikosi, Shirikisho halijatangaza mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake kwa sasa. Hata hivyo, imeelezwa kuwa endapo kutakuwa na mabadiliko, taarifa rasmi zitatolewa kwa umma.

Stars kuondoka kuelekea Morocco

Katika hatua nyingine, timu ya Taifa ya Tanzania itaondoka leo saa 5:00 usiku kuelekea Morocco kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa.

Timu hiyo itacheza dhidi ya Uganda tarehe 5 Juni, kabla ya kumenyana na Rwanda tarehe 9 Juni.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.