Mbappe amepishana na gari la mshahara PSG

Joel JJ By Joel JJ • 31st May 2026


Mbappe amepishana na gari la mshahara PSG

Klabu ya Paris Saint-Germain imeendelea kuandika historia mpya barani Ulaya baada ya kutwaa taji la pili mfululizo la UEFA Champions League, kufuatia ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Arsenal FC katika fainali kali iliyochezwa Mei 30, 2026 jijini Budapest.

Mchezo huo uliisha kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, kabla ya PSG kuibuka na ubingwa kupitia mikwaju ya penalti, ushindi ambao uliwafanya kuendelea kutawala soka la Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo.

Ushindi wa PSG na historia mpya Ulaya

PSG sasa ni moja ya timu chache katika historia ya kisasa ya Champions League kutetea ubingwa wao kwa mafanikio, jambo linalothibitisha mabadiliko makubwa ndani ya klabu hiyo baada ya kujijenga upya.

Ushindi huu pia unaweka PSG katika kundi la vilabu vilivyoonyesha uthabiti mkubwa katika mashindano ya Ulaya, huku mashabiki wao wakisherehekea mafanikio makubwa ya mfululizo.

Hadithi ya Mbappé na Real Madrid

Wakati PSG ikiendelea kung’ara, macho ya dunia ya soka bado yapo kwa nyota wa Ufaransa Kylian Mbappé, ambaye alihamia katika klabu ya Real Madrid CF akiamini kuwa ndiko atakakopata nafasi kubwa ya kushinda tena Champions League na kushinda tuzo ya Ballon d'or.

Hata hivyo, hali imekuwa tofauti, waswahili wanasema amepishana na gari la mshahara..! presha imeendelea kumkabili Madrid kutokana na matarajio makubwa ya mashabiki na matokeo yasiyo thabiti.

Msimu huu Real Madrid haikushinda taji lolote huku takwimu zikionyesha tangu Mbappe atue kwa mabingwa hao wa kihistoria Ulaya, mambo yanawaendelea kombo hadi kupelekea baadhi ya mashabiki kushinikiza aondoke

Mgogoro wa mashabiki Real Madrid

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Real Madrid wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo, wakimtaja Mbappe kama mmoja wa wachezaji wanaoikwamisha timu hiyo wakimuita 'dikteta'

Kampeni ya kutaka Mbappe aondoke Real Madrid imeendeshwa mitandaoni ambapo takribani mashabiki 700M kote Duniani wakisaini petisheni hiyo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.