Manara kuzisemea timu zote za Taifa Tanzania

Joel JJ By Joel JJ • 28th May 2026


Manara kuzisemea timu zote za Taifa Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Paul Makonda, amemteua Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za Tanzania katika hatua inayolenga kuboresha mawasiliano na uhamasishaji wa michezo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 28, 2026 katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Waziri Makonda amesema uteuzi huo unalenga kuongeza nguvu katika usimamizi wa taswira na taarifa za timu za Taifa, hususan timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania.

Mh Makonda amesema Haji Manara atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambalo litasimamia utekelezaji wa majukumu yake katika kuratibu Mawasiliano ya timu zote za Taifa.

Lengo la uteuzi

Makonda amesema lengo kuu la uteuzi huo ni kuhakikisha taarifa za timu za Taifa zinawafikia wananchi kwa wakati, kwa uwazi na kwa ufanisi zaidi, pamoja na kuongeza hamasa kwa mashabiki kuelekea mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Aidha, uteuzi huo unahusisha timu zote za Taifa, zikiwemo za vijana na wanawake, chini ya mfumo wa usimamizi wa Baraza la Michezo la Taifa.

Manara amewahi kuzitumikia klabu za Yanga na Simba katika nafasi za usemaji kwa mafanikio makubwa. 


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.