Barcelona hawatanii: Wamnasa Anthony Gordon katika dili la Euro milioni 70

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th May 2026


Barcelona hawatanii: Wamnasa Anthony Gordon katika dili la Euro milioni 70

FC Barcelona wanaendelea kuonyesha kwamba msimu huu wa usajili hawako tayari kufanya mzaha. Klabu hiyo ya Catalonia sasa iko hatua kubwa karibu kumsajili nyota wa Newcastle United, Anthony Gordon, katika dili linalokadiriwa kufikia zaidi ya €70 milioni.

Kwa mujibu wa taarifa, Barcelona na Newcastle wamefikia makubaliano ya awali kuhusu ada ya uhamisho, huku mchezaji huyo akishafikia pia makubaliano binafsi na klabu hiyo ya Hispania.

Ripoti zinaeleza kuwa Gordon anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Barcelona kabla ya kukamilisha uhamisho wake, jambo linaloashiria kuwa dili hilo limeingia hatua za mwisho. Barcelona wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo kwa muda kutokana na uwezo wake wa kucheza pembeni na pia kuongeza kasi ya mashambulizi.

Sababu kuu inayowavutia Barcelona ni uwezo wa Gordon kucheza kwa intensity kubwa, kasi ya kushambulia, na flexibility ya kucheza nafasi mbalimbali za mbele. Kocha Hansi Flick anaamini mchezaji huyo anaweza kusaidia kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji pamoja na kuwa mbadala wa haraka wa wachezaji kama Raphinha.

Kwa upande wa Newcastle, uamuzi wa kumuuza Gordon unaonekana kuwa sehemu ya mpango wa kuimarisha kikosi kwa fedha kubwa zitakazotokana na mauzo hayo, hasa baada ya msimu wenye matokeo yasiyo thabiti kwa klabu hiyo.

Hata hivyo, ingawa makubaliano yanaonekana kuwa karibu kukamilika, hatua za mwisho kama vipimo vya afya na kusaini mkataba bado zinahitajika kabla ya kutangazwa rasmi.

Kilicho wazi ni kwamba Barcelona hawatanii, wanajenga kikosi chenye kasi, nguvu na ubora wa muda mrefu, na Anthony Gordon anaonekana kuwa sehemu muhimu ya mipango hiyo mpya ya Camp Nou.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.