KMC wafikia rekodi mbaya ya Kengold Fc Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th May 2026


KMC wafikia rekodi mbaya ya Kengold Fc Ligi Kuu

Klabu ya KMC FC imeifikia rasmi rekodi mbaya iliyokuwa inashikiliwa na Kengold FC ya kupoteza michezo 20 katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ya NBC.

KMC wamefikisha idadi hiyo baada ya jana kuchapwa mabao 3-0 na Azam FC wakipoteza mechi yao ya 20 msimu huu, huku wakiwa bado na michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2025/26.

Kengold waliweka rekodi hiyo misimu miwili iliyopita baada ya kupoteza mechi 20 katika michezo 30 kabla ya kushuka daraja.

Mpaka sasa KMC wamecheza mechi 25 ambapo wameshinda michezo miwili pekee, kutoka sare mara tatu na kupoteza michezo 20, hali inayozidi kuweka matumaini yao ya kubaki ligi kuu katika mazingira magumu.

Matokeo hayo yameifanya klabu hiyo kuwa katika hatari kubwa ya kushuka daraja kwenda Championship msimu ujao, huku wachambuzi wa soka wakieleza kuwa KMC wanahitaji muujiza kuweza kunusurika kushuka daraja.

Ratiba iliyosalia kwa KMC inaonyesha kuwa bado wana kazi ngumu mbele yao, ambapo watakutana na Coastal Union, TRA United, Namungo FC, Mashujaa FC pamoja na Simba SC.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.