Fei Toto ameshindikana, apewe tuzo yake mapema

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th May 2026


Fei Toto ameshindikana, apewe tuzo yake mapema

Jana Azam FC iliendeleza ubabe uwanja wa Azam Complex wakiwachapa vibnde KMC mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Mabao ya Azam Fc katika mchezo huo yalifungwa na Feisal Saum 'Fei Toto' aliyefunga mabao mawili huku bao la tatu likifungwa na Yoro Diaby.

Fei Toto ameendelea kuwa mtambo wa kuzalisha mabao katika kikosi cha Azam Fc msimu huu akiwa tayari amehusika katika mabao 22.

Amefunga mabao 14 na kutoa pasi nane za usaidizi wa mabao. Mchezaji anayemfuatia ni Allan Okello wa Yanga ambaye amefunga mabao 11 na pasi 7 za usaidizi wa mabao akiwa amehusika kwenye mabao 17.

Ni wazi kama ligi inamalizika leo, Fei Toto anastahili tuzo ya mchezaji bora wa msimu 'MVP' na ufungaji bora pia.

Ni msimu wa tatu mfululizo Fei Toto ameendelea kuwa mtambo wa kuzalisha mabao Azam FC.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.