Barcelona yatawala kikosi cha Hispania kombe la Dunia

Joel JJ By Joel JJ • 25th May 2026


Barcelona yatawala kikosi cha Hispania kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Hispania (Spain) imetangaza rasmi kikosi chake cha wachezaji 26 kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, huku klabu ya FC Barcelona ikitawala kwa kutoa wachezaji wanane (8) kwenye kikosi hicho cha mwisho.

Kocha wa Hispania, Luis de la Fuente, ametaja kikosi chenye mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu, kikilenga kuipa Hispania nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa dunia.

Hispania iko katika Kundi H pamoja na Uruguay, Saudi Arabia na Cape Verde, na itaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia tarehe 15 Juni 2026 dhidi ya Cape Verde.


BARCELONA YATAWALA KIKOSI CHA LA ROJA

Barcelona imekuwa klabu inayoongoza kwa kuchangia wachezaji kwenye kikosi hicho, ikiwa na nyota muhimu wanaounda msingi wa timu ya taifa.

Wachezaji 8 wa Barcelona walioitwa ni:

  • Lamine Yamal
  • Pedri
  • Gavi
  • Dani Olmo
  • Ferran Torres
  • Pau Cubarsí
  • Eric García
  • Joan García

Katika kikosi hicho pia hakuna mchezaji hata mmoja wa klabu ya Real Madrid.


KIKOSI KAMILI CHA HISPANIA (WACHEZAJI 26)

MAKIPA

  • Unai Simón (Athletic Club)
  • David Raya (Arsenal)
  • Joan García (Barcelona)

MABEKI

  • Marc Cucurella (Chelsea)
  • Alejandro Grimaldo (Bayer Leverkusen)
  • Pau Cubarsí (Barcelona)
  • Aymeric Laporte (Athletic Club)
  • Eric García (Barcelona)
  • Marc Llorente (Atlético Madrid)
  • Pedro Porro (Tottenham)
  • Marc Pubill (Atlético Madrid)

VIUNGO

  • Rodri (Manchester City)
  • Pedri (Barcelona)
  • Gavi (Barcelona)
  • Mikel Merino (Arsenal)
  • Martín Zubimendi (Arsenal)
  • Fabián Ruiz (PSG)
  • Álex Baena (Atlético Madrid)

WASHAMBULIAJI

  • Lamine Yamal (Barcelona)
  • Nico Williams (Athletic Club)
  • Ferran Torres (Barcelona)
  • Dani Olmo (Barcelona)
  • Mikel Oyarzabal (Real Sociedad)
  • Yeremy Pino (Crystal Palace)
  • Borja Iglesias (Celta Vigo)
  • Víctor Muñoz (Osasuna)

  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.