Fei Toto, Nado waiadhibu Prisons Azam Complex

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd May 2026


Fei Toto, Nado waiadhibu Prisons Azam Complex

Azam Fc imeendeleza ubabe dimba la Azam Complex ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC kukamilisha raundi ya 24.

Alikuwa ni Feisal Salum 'Fei Toto' na Iddi Nado waliofunga mabao ya Azam Fc na kuhakikisha alama tatu zinasalia Msimbazi.

Fei Toto ameendelea kujiimarisha kwenye mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 12 huku Nado nae akifikisha mabao 8.

Sio matokeo mazuri kwa upande wa Tanzania Prisons kwani wanaendelea kusalia nafasi ya 15 wakiwa kwenye eneo la kuteremka daraja.

Azam Fc imefikisha alama 49 ikiendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa kimahesabu kwani wamechwa alama nane na vinara wa ligi, Yanga


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.