Shirikisho la Soka la Senegal limetangaza rasmi kikosi cha wachezaji 26 kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, kikiongozwa na nahodha na nyota wake wa ushambuliaji Sadio Mané.
Kikosi hicho kimetangazwa na kocha mkuu Pape Thiaw, kikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa pamoja na vipaji chipukizi vinavyocheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya na Asia.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, kikosi hicho kinajumuisha makipa watatu, mabeki, viungo na washambuliaji wakikamilisha wachezaji 26 walioteuliwa kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.
MAKIPA
- Édouard Mendy (Al-Ahli)
- Yehvann Diouf (Nice)
- Mory Diaw (Le Havre)
MABEKI
- Kalidou Koulibaly (Al-Hilal)
- Moussa Niakhaté (Lyon)
- Mamadou Sarr (Chelsea)
- Antoine Mendy (Nice)
- El Hadji Malick Diouf (West Ham United)
- Abdoulaye Seck (Maccabi Haifa)
- Ismail Jakobs (Monaco)
- Krepin Diatta (Monaco)
- Nobel Mendy (Rayo Vallecano)
VIUNGO
- Idrissa Gana Gueye (Everton)
- Pape Matar Sarr (Tottenham)
- Pape Gueye (Villarreal)
- Cheikhou Kouyaté
- Nampalys Mendy
- Pathé Ciss
WASHAMBULIAJI
- Sadio Mané (Al-Nassr)
- Nicolas Jackson (Chelsea)
- Ismaïla Sarr (Crystal Palace)
- Iliman Ndiaye (Everton)
- Boulaye Dia (Lazio)
- Habib Diallo
Senegal ipo katika kundi I pamoja na:
- France
- Senegal
- Norway
- Iraq
MECHI YA KWANZA YA SENEGAL
- France vs Senegal
- Tarehe: 16 Juni 2026
- Uwanja: New York/New Jersey Stadium (MetLife Stadium)
- Saa: takribani 3:00 usiku (ET)



