Vita ya ubingwa ligi kuu Misri kuhitimishwa leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th May 2026


Vita ya ubingwa ligi kuu Misri kuhitimishwa leo

Hatma ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri itafahamika leo usiku baada ya mzunguko wa mwisho wa msimu kupigwa kwa wakati mmoja katika viwanja vitatu tofauti, huku ushindani ukiwa mkali kati ya timu tatu zinazoongoza msimamo.

Mechi zote zimepangwa kuanza saa 2:00 usiku kwa saa za Cairo, katika mazingira yanayotarajiwa kuwa ya ushindani mkali na presha kubwa kwa timu zote zinazowania taji.

Mechi za mwisho za msimu

Katika michezo hiyo ya mwisho:

  • Al Ahly watavaana na Al Masry
  • Pyramids FC watacheza dhidi ya Smouha SC
  • Zamalek SC watakabiliana na Ceramica Cleopatra FC

Matokeo ya mechi hizi tatu yataamua bingwa wa msimu huu, huku ushindani ukiwa bado wazi kwa timu zote tatu zilizo kwenye nafasi za juu.

Msimamo wa ligi kabla ya mechi za mwisho

Kabla ya michezo hiyo, msimamo wa ligi ulikuwa kama ifuatavyo:

  1. Zamalek SC – pointi 53 (michezo 25)
  2. Pyramids FC – pointi 51 (michezo 25)
  3. Al Ahly – pointi 50 (michezo 25)

Mahesabu ya ubingwa

Zamalek SC wanahitaji angalau ushindi au sare kuhakikisha wanabaki kileleni bila kutegemea matokeo ya wapinzani wao.
Pyramids FC wanahitaji ushindi pamoja na matokeo yasiyokuwa mazuri kwa Zamalek ili kutwaa ubingwa.
Kwa upande wao, Al Ahly wana nafasi ya kutwaa taji endapo Zamalek watapoteza na Pyramids FC watashindwa kushinda.

Mpangilio wa kipekee wa ubingwa

Shirikisho la soka la Misri limeweka utaratibu wa kipekee wa kuonesha ubingwa, ambapo kombe la ligi litawekwa kwenye ndege maalum itakayokuwa ikizunguka kati ya viwanja vitatu vinavyopokea michezo ya mwisho.

Ndege hiyo itakuwa ikizunguka Cairo International Stadium, Air Defense Stadium na Borg El Arab Stadium, ikisubiri kutua kwenye uwanja wa timu itakayothibitishwa kuwa bingwa mara baada ya mechi kumalizika.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.