Ligi Kuu, mechi za leo Jumatano May 20

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th May 2026


Ligi Kuu, mechi za leo Jumatano May 20

Ligi Kuu ya NBC imeingia mzunguuko wa 24 ambapo leo mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Baada ya kutupwa nje ya michuano kombe la CRDB kwa kipigo cha aibu cha mabao 4-0 dhidi ya Simba, watoza ushuru wa TRA United leo wako dimba la Sheikh Amri Abeid kuikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.

KMC ambayo inahitaji muujiza kunusurika kushuka daraja, watakuwa dimba la KMC Complex kuikabili Pamba Jiji mchezo utakaopigwa saa 12 jioni.

Baada ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kutoka kifungoni, wenyeji Dodoma Jiji watawakaribisha maafande wa Mashujaa Fc katika mchezo utakopigwa saa 3 usiku.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.