Shirikisho la soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) limetangaza rasmi kikosi cha wachezaji 26 kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, huku mshambuliaji nyota wa Pyramids Fc Fiston Mayele akijumuishwa kwenye orodha hiyo muhimu.
Kocha Sébastien Desabre ametegemea mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu barani Ulaya pamoja na mastaa wanaofanya vizuri Afrika na Mashariki ya Kati, huku DR Congo ikirejea kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.
Mayele, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Pyramids FC ya Misri, amekuwa katika kiwango bora msimu huu baada ya kufunga mabao muhimu kwenye michuano ya ndani na ya Afrika.
Mbali na Mayele, majina makubwa yaliyoitwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Yoane Wissa, Cedric Bakambu, Aaron Wan-Bissaka, Chancel Mbemba na Simon Banza.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano, DR Congo ipo kundi moja na Portugal, Colombia pamoja na Uzbekistan. Leopards wanatarajia kutumia ushindani huo kuonyesha ubora wao duniani baada ya kusubiri zaidi ya miaka 50 kurejea kwenye Kombe la Dunia.
Kikosi Kamili cha DR Congo Kombe la Dunia 2026
Makipa
- Lionel Mpasi
- Timothé Fayulu
- Matthieu Epolo
Mabeki
- Aaron Wan-Bissaka
- Axel Tuanzebe
- Chancel Mbemba
- Dylan Batubinsika
- Rocky Bushiri
- Arthur Masuaku
- Joris Kayembe
- Steve Kapuadi
- Gedeon Kalulu
Viungo
- Samuel Moutoussamy
- Edo Kayembe
- Charles Pickel
- Noah Sadiki
- Ngal’ayel Mukau
- Gael Kakuta
Washambuliaji
- Fiston Mayele
- Yoane Wissa
- Cedric Bakambu
- Simon Banza
- Theo Bongonda
- Meshack Elia
- Nathanael Mbuku
- Brian Cipenga



