Coastal Union yatangulia nusu fainali kombe la CRDB

Joel JJ By Joel JJ • 16th May 2026


Coastal Union yatangulia nusu fainali kombe la CRDB

Coastal Union imetinga nusu fainali ya kombe la CRDB baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Singida BS kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana hatua iliyopelekea mshindi kuamuliwa na mikwaju ya penati.

Singida BS watajilaumu wenyewe kwa kukosa ushindi ndani ya dakika 90 kwani katika dakika za lala salama walipata mkwaju wa penati ambao Ibrahim Imoro alikosa.

Coastal Union sasa wanasubiri mshindi wa mchezo mwingine wa robo fainali kati ya Simba dhidi ya TRA United kuelekea hatua ya nusu fainali.

 


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.