Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo nne mfululizo za nyota wa mchezo ligi kuu ya NBC msimu huu.
Chama amechukua tuzo za nyota wa mchezo katika mechi dhidi ya Yanga, JKT Tanzania, Tanzania Prisons na Mashujaa Fc.
Katika mechi hizo Chama amefunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao.
Mpaka sasa Chama mefunga mabao manane huku akitoa pasi nne za mabao.
Hii ni rekodi msimu huu kwa Chama kufikia mafanikio hayo.




