Mabao mawili ya dakika za lala salama yameihakikishia Azam Fc kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Azam Complex.
Mabao ya Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga kwa kichwa dakika ya 90 na Japhet Kitambala aliyefunga dakika 93 yalizima kabisa ndoto ya Pamba Jiji kuondoka na angalau alama moja dimba la Azam Compelex.
Ulikuwa mchezo ambao Azam Fc walitawala kwa muda mwingi lakini nidhamu ya safu ya ulinzi ya Pamba Jiji iliwaweka salama kwa muda mwingi wa mchezo kabla ya kupoteza umakini kwenye dakika za lala salama.
Ushindi huo unaifanya Azam Fc ifikishe alama 46, kimahesabu wamerejea kwenye mbio za ubingwa kwani wako nyuma ya vinara wa ligi hiyo Yanga kwa tofauti ya alama nane.



