Baada ya Yanga kukubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji, wamewapa nafasi watani zao Simba kuwasogelea karibu zaidi kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Simba leo itakuwa ugenini mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Alama tatu kwa Mnyama zitamaanisha Wekundu hao wa Msimbazi watafikisha alama 52 na hivyo kuwa tofauti ya alama mbili tu dhidi ya Yanga ambao bado iko kileleni ikiwa na alama 54 baada ya mechi 23.
Simba ilitua Kigoma jioni ya Jumatano timu hiyo ikikamilisha maandalizi yake yote kuelekea mchezo huo jijini Dar es salaam.
Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola amesema wanatambua Mashujaa Fc sio timu nyepesi hasa inapocheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu.



