Ligi Kuu ya NBC, mechi mbili kupigwa leo May 12

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th May 2026


Ligi Kuu ya NBC, mechi mbili kupigwa leo May 12

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 23 ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa.

Baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, walima alizeti wa Singida BS watashuka tena uwanja wao wa nyumbani, Airtel Mtipa kuikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa saa 8 mchana.

Namungo Fc chini ya kocha Juma Mgunda walilazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc.

Bado mambo ni magumu kwa Mgunda na vijana wake kwani wamecheza takribani mechi 12 bila ya ushindi.

Saa 10 jioni TRA United wataikaribisha JKT Tanzania katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali.

Ni vita ya kuwania nne bora, je TRA United wataendeleza ubabe wao Sheikh Amri Abeid baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopita?

Hata hivyo ni wazi haitakuwa mechi rahisi mbele ya maafande wa JKT Tanzania ambao msimu huu wameonyesha kuitaka nafasi ya nne iki wapate nafasi ya kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.