Barcelona kubeba taji la La Liga mbele ya Real Madrid leo?

Joel JJ By Joel JJ • 10th May 2026


Barcelona kubeba taji la La Liga mbele ya Real Madrid leo?

Klabu ya FC Barcelona ipo hatua moja pekee kutwaa ubingwa wa La Liga kwa msimu wa pili mfululizo huku ikihitaji sare au ushindi katika mchezo wa dabi dhidi ya Real Madrid utakaopigwa leo Jumapili saa 4 usiku.

Mchezo huo wa El Clásico unasubiriwa kwa hamu kubwa duniani kote kutokana na umuhimu wake katika kuamua hatima ya ubingwa wa Hispania msimu huu.

Barcelona wanaingia katika pambano hilo wakiwa kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo ya hivi karibuni. Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Hansi Flick kimekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo na sasa kinahitaji pointi moja pekee kuthibitisha ubingwa.

Iwapo Barcelona watapata sare au ushindi dhidi ya mahasimu wao wa jadi Real Madrid, watatwaa rasmi taji la La Liga mbele ya wapinzani wao hao jambo ambalo litakuwa pigo kubwa kwa Madrid.

Nyota wa Barcelona akiwemo Robert Lewandowski anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji sambamba na vijana Pedri, Gavi na Dani Olmo ambao wamekuwa muhimu katika mafanikio ya timu hiyo msimu huu.

Kwa upande wa Real Madrid, mchezo huo ni wa lazima kushinda ili kulinda heshima ya klabu hiyo. Hata hivyo, timu hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto za majeraha pamoja na presha ya matokeo yasiyoridhisha katika baadhi ya michezo ya hivi karibuni.

Mashabiki wa Barcelona tayari wanaonekana kujiandaa kwa sherehe kubwa iwapo timu yao itafanikiwa kutwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao wa jadi katika mchezo huo mkubwa.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.