Varverde ataikosa El Classico Jumapili

Joel JJ By Joel JJ • 8th May 2026


Varverde ataikosa El Classico Jumapili

Kiungo wa kati wa Real Madrid, Federico Valverde, atakosa mchezo wa El Clásico dhidi ya FC Barcelona utakaopigwa Jumapili mwishoni mwa wiki kutokana na jeraha la kichwa alilolipata kufuatia tukio la ugomvi katika kambi ya mazoezi ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu na vyombo mbalimbali vya habari, Valverde aliumia baada ya mvutano mkali uliotokea kati yake na kiungo mwenzake Aurélien Tchouaméni wakati wa mazoezi ya kikosi cha kwanza katika uwanja wa Valdebebas.

Tukio hilo linasemekana lilianza kama makabiliano ya kawaida ya mazoezi kabla ya kugeuka na kuwa mzozo mkali uliopelekea Valverde kupata jeraha la kichwa lililohitaji matibabu ya haraka kutoka kwa timu ya madaktari wa klabu.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi, imebainika kuwa mchezaji huyo atahitaji muda wa mapumziko ya takribani wiki moja hadi mbili, hali inayomuweka nje ya mchezo muhimu wa El Clásico.

Kukosekana kwa Valverde ni pigo kubwa kwa Real Madrid kutokana na umuhimu wake katika safu ya kiungo, hasa katika mechi zenye ushindani mkubwa dhidi ya wapinzani wao wakuu Barcelona.

Wakati huo huo, uongozi wa klabu hiyo unaendelea kuchunguza tukio hilo la mazoezini huku ukielezwa kutoridhishwa na tabia ya utovu wa nidhamu uliosababisha mchezaji wake muhimu kuumia kabla ya mchezo mkubwa.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.