Bao la Chama linatazamwa kila kona, kuwania tuzo FIFA?

Joel JJ By Joel JJ • 7th May 2026


Bao la Chama linatazamwa kila kona, kuwania tuzo FIFA?

Goli lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Yanga SC limeendelea kuzua mjadala mkubwa mitandaoni na miongoni mwa wadau wa soka, likipigiwa chapuo kuwa huenda likafaa kuwania tuzo ya FIFA Puskás inayotolewa kwa goli bora la mwaka.

Goli hilo ambalo lilifungwa katika mchezo mkali na wenye ushindani mkubwa kati ya vigogo hao wa soka nchini Tanzania, limeelezwa na mashabiki pamoja na wachambuzi kuwa la kiufundi, la kipekee na lenye ubunifu wa hali ya juu, hali iliyolifanya kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuvuta hisia za wadau wa soka ndani na nje ya Afrika.

Baadhi ya wapenzi wa soka wamekuwa wakilitaja goli hilo kama mojawapo ya magoli bora kuwahi kufungwa katika ligi ya ndani, huku wakiamini linaweza kuingia katika orodha ya mapendekezo ya tuzo ya kimataifa ya Puskás iwapo litapitia vigezo na mchakato rasmi wa uteuzi wa FIFA.

Inaelezwa pia kuwa wadau mbalimbali wa soka pamoja na uongozi wa klabu ya Simba SC wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwitikio wa kimataifa kuhusu goli hilo, ambalo limeendelea kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni na mitandao ya kijamii, huku likipata watazamaji wengi zaidi mtandaoni.

Chama alifunga bao hilo dakika ya 8 ya mchezo, likiwa ni bao la pili kwa Simba SC katika Kariakoo Derby dhidi ya Yanga SC, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.