Vilabu vikubwa vya soka barani Ulaya vinaendelea kujipanga kuelekea dirisha la usajili wa majira ya kiangazi huku tetesi mbalimbali zikionyesha uwezekano wa nyota kadhaa kubadili timu mwishoni mwa msimu huu.
Manchester United wanatajwa kupanga kufanya maboresho makubwa katika eneo la kiungo, ambapo taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo iko tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 150 kusajili wachezaji wapya.
Majina yanayotajwa kwenye mipango ya United ni pamoja na Morgan Rogers wa Aston Villa pamoja na Mateus Fernandes. Ripoti hizo pia zinaeleza kuwa United wanaweza kumuuza Manuel Ugarte ili kupata fedha za usajili huo.
Chanzo: Sky Sports
Kwa upande wa Hispania, Barcelona wanaendelea kutafuta maboresho ya safu ya ulinzi huku wakimtazama kwa karibu Wesley Fofana wa Chelsea.
Inaelezwa kuwa Fofana amewekwa kama mbadala wa Alessandro Bastoni wa Inter Milan iwapo dili hilo litashindikana. Chelsea wanatajwa kuhitaji euro milioni 30 kumuachia beki huyo wa Ufaransa.
Chanzo: Barca Blaugranes
Liverpool nao wanaendelea kuimarisha mipango yao ya usajili kwa kuwafuatilia wachezaji kadhaa wa safu ya ushambuliaji na ulinzi.
Majina yanayotajwa katika rada ya Liverpool ni Yan Diomande, Bradley Barcola, Marcos Senesi pamoja na Denzel Dumfries.
Chanzo: Liverpool Offside
Nchini Ujerumani, Bayern Munich wameongeza juhudi za kumshawishi Anthony Gordon kuondoka Newcastle United.
Ripoti zinaeleza kuwa Bayern tayari wamempa ofa ya mkataba wa miaka mitano, huku Newcastle wakihitaji kati ya pauni milioni 75 hadi 80 kwa ajili ya kumuachia nyota huyo wa England.
Chanzo: Coming Home Newcastle
Wakati huo huo, mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez anaripotiwa kuwa tayari kuondoka Al Hilal chini ya mwaka mmoja tangu ajiunge na klabu hiyo.
Nyota huyo wa zamani wa Liverpool anatajwa kuvutiwa na uwezekano wa kurejea Ligi Kuu England baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu Saudi Arabia.
Chanzo: Talksport
Kwa upande mwingine, Aston Villa wanatajwa kufufua nia ya kumsajili mshambuliaji Jonathan David wa Juventus katika dirisha lijalo la usajili.
Chanzo: Bavarian Football Works



