Winga AFAD-Plateau katika rada za Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th May 2026


Winga AFAD-Plateau katika rada za Yanga

Klabu ya Yaanga imeingia katika mbio za kumsaka winga wa kulia wa klabu ya AFAD-Plateau, Amani Kouadiokan Michel Breygeneve (27), ambaye amekuwa na msimu bora nchini Ivory Coast.

Baada ya Ecua Celestin kushindwa kuwashawishi Wananchi na kupelekea akatolewa kwa mkopo JS Kabylie huku mbadala wake Buba Jammeh nae akishindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza, Yanga imejipanga kurudi sokoni kuimarisha eneo lake la washambuliaji wa pembeni.

Kwa mujibu wa taarifa za usajili, Yanga inafuatilia kwa karibu huduma ya mchezaji huyo ambaye amejipambanua kama mmoja wa wachezaji hatari zaidi katika ligi ya Ivory Coast msimu huu.

Breygeneve amekuwa katika kiwango cha juu akiwa miongoni mwa wafungaji bora, akifanikiwa kufunga mabao 10 na kutoa asisti 6 katika mechi 24 alizocheza msimu huu. Takwimu hizo zimemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia macho ya timu mbalimbali barani Afrika.

Mchezaji huyo anatajwa kuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, jambo linalomfanya kuwa tishio kwa mabeki wa pembeni. Aidha, anasifika kwa kasi na nguvu anazotumia anaposhambulia, sifa zinazomuweka kwenye daraja la wachezaji wanaoweza kutumika kwenye nafasi zaidi ya moja katika safu ya ushambuliaji.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.