Baada ya kutoana jasho kwenye mchezo wa Kariakoo Derby May 03 uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kumalizika kwa matokeo ya sare y mabao 2-2, klabu za Simba na Yanga leo tena zinashuka viwanjani katika mechi za raundi ya 21 ligi kuu ya NBC.
Mabingwa watetezi, Yanga wao watashuka uwanja wa KMC Complex kumenyana na 'vibonde' KMC katika mchezo ambao Yanga wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Ni vita kati ya vinara wa ligi dhidi ya timu inayoburuza mkia, ikiwa imekusanya alama 9 tu kutoka michezo 20.
Nao Simba wao watakuwa na 'shughuli pevu' pale Jeshini Meja Jenerali Isamuhyo watakapokanbiliana na JKT Tanzania.
Ni mchezo unaozikutanisha timu mbili zinazotumia uwanja wa Isamuhyo kama uwanja wa nyumbani, unaweza kusema ni dabi ya Isamuhyo.
Mchezo wa mwisho siku ya leo ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa uwanja wa Azam Complex.




