Singida BS, Fountain Gate zapeta nyumbani Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th May 2026


Singida BS, Fountain Gate zapeta nyumbani Ligi Kuu

Ligi Kuu Tanzania Bara iliendelea leo Jumanne, Mei 5, 2026 mechi za raundi ya 21 zikianza kupigwa.

Katika mchezo uliochezwa uwanja wa Airtel, Singida Black Stars waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Pamba Jiji.

Nyota wa mchezo huo alikuwa Ndumumwe Mosi aliyefunga mabao mawili na kuiongoza timu yake kupata ushindi muhimu. Bao la tatu la Singida lilifungwa na Horso Malonga, akiihakikishia timu yake pointi tatu muhimu.

Kwa upande wa Pamba Jiji, bao lao pekee lilifungwa na Herry Luongwa katika dakika ya 90, likiwa la kufutia machozi baada ya kuchelewa kuamka katika mchezo huo.

Katika mchezo mwingine wa kusisimua uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mkoani Arusha, Fountain Gate waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Coastal Union.

Mabao ya Fountain Gate yalifungwa na Chukwunonye McDonald, Henry David pamoja na Ismail Kader, waliotumia vyema nafasi walizozipata.

Coastal Union walijibu mapigo kupitia kwa Shiza Kichuya na Meshack Mwamita, lakini juhudi zao hazikutosha kuzuia kipigo hicho, huku wakishindwa kurejea kwenye mchezo licha ya kupambana hadi dakika za mwisho.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.