Klabu ya Athletic Club imemtangaza rasmi Edin Terzic kuwa kocha mkuu mpya, akichukua mikoba ya Ernesto Valverde. Terzic amesaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo hadi june 2028, katika viunga vya dimba la san mames.
Kocha huyo raia wa ujerumani anajiunga na bilbao, ambapo aliwahi kuiongoza timu hiyo hadi kufika fainali ya UEFA Champions League. Uzoefu huo unampa hadhi ya kuaminiwa kuleta mabadiliko na ushindani mpya ndani ya kikosi cha Athletic club.
Kuondoka kwa Valverde kunatajwa kuchochewa na sababu kadhaa, ikiwemo matokeo yasiyoridhisha pamoja na ukosefu wa maendeleo ya wazi ya timu katika kipindi cha hivi karibuni. Uongozi wa klabu uliamua kufanya mabadiliko ili kurejesha ari ya ushindani wa timu na matarajio ya mashabiki wa Bilbao.
kwa upande wake, Terzic anatarajiwa kuleta mbinu za kisasa, uwezzo wa kuunganisha wachezaji na ari mpya ya ushindani. Akiwa anajulikana kwa uwezo wake wa kuhamasisha timu na kujenga mshikamano, macho yote sasa yako kwake kuona kama ataweza kuirejesha Athletic Clib katoka ubora wake unaotarajiwa.
kwa ujumla, uteuzi huu unaashiria mwanzo wa safari mpya kwa Bilbao, huku mashabiki wakisubiri kuona matokeo ya uongozi mpya chini ya terzic kutoka dortmund hadi Bilbao, changamoto mpya imeanza rasmi.



