Real Madrid waichelewesha Barcelona kutangaza ubingwa La Liga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th May 2026


Real Madrid waichelewesha Barcelona kutangaza ubingwa La Liga

Real Madrid wamefanikisha kazi yao ya kuchelewesha sherehe za ubingwa kwa wapinzani wao wakubwa Barcelona baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Espanyol Jumapili, Mei 3, 2026.

Katika mechi hiyo ya La Liga iliyochezwa kwa ushindani mkali, Real Madrid walionyesha uimara wao na kutumia nafasi walizopata, Vinicios Junior akifunga mabao yote na kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu muhimu ugenini.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Barcelona bado hawajaweza kutangazwa mabingwa rasmi wa ligi hiyo, licha ya kuwa karibu na taji hilo msimu huu.

Madrid walionekana kuingia uwanjani wakiwa na dhamira moja kuu kutokubali kupoteza au kutoa nafasi yoyote ambayo ingewasaidia Barcelona kutwaa ubingwa mapema.

Mashabiki na wachambuzi wa soka nchini Hispania wanasema matokeo hayo yanaongeza ladha ya ushindani kuelekea mchezo unaosubiriwa kwa hamu wa El Clásico, ambao sasa unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuamua hatima ya ubingwa wa ligi msimu huu.

Kama Real Madrid watakosa ushindi kwenye El Classico basi Barcelona watatawazwa kuwa mabingwa wa La Liga kwa msimu wa pili mfululizo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.