Fei Toto hakamatiki, afunga mawili Azam Fc ikiichapa Mtibwa Sugar 3-0

Joel JJ By Joel JJ β€’ 2nd May 2026


Fei Toto hakamatiki, afunga mawili Azam Fc ikiichapa Mtibwa Sugar 3-0

Leo Jumamosi, Mei 02, 2026, mashabiki wa soka nchini walishuhudia michezo miwili ya ligi kuu ya NBC, yenye ushindani mkali huku timu zikionyesha dhamira ya kusaka alama muhimu.

Katika dimba la KMC Complex, mapema Mtibwa Sugar walikaribisha Azam FC katika mchezo uliotawaliwa na wageni. Azam FC waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0, wakionyesha ubora mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Nyota wa mchezo huo alikuwa Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, aliyefunga mabao mawili na pia kutoa pasi ya bao kwa Japhet Kitambala.

Kwa mafanikio hayo, Feisal sasa anaongoza orodha ya wafungaji bora akifikisha mabao 9, huku pia akiwa ametoa pasi 8 za mabao, takwimu zinazoonyesha mchango wake mkubwa ndani ya kikosi cha Azam FC kwa msimu wa tatu mfululizo.

Wakati huo huo, katika mchezo mwingine uliokuwa na ushindani mkubwa, Coastal Union waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars. Licha ya kucheza pungufu baada ya kupata kadi nyekundu kwa mlinda lango, Coastal Union waliweza kuhimili presha na kuhakikisha wanabeba alama zote tatu.

Mabao ya Coastal Union yalifungwa na Bakari Msimu pamoja na Mabad Maulid aliyefunga kwa njia ya penati. Kwa upande wa Singida BS, bao lao pekee lilifungwa na Emmanuel Keyekeh kupitia mkwaju wa penati.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.