Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili za raundi ya 20 zitapigwa jijini Dar es salaam na mkoani Tanga.
Mchezo wa mapema saa 10 jioni, Mtibwa Sugar wataikaribisha Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.
Baada ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kufungiwa na TFF, Mtibwa Sugar wamechagua kutumia uwanja wa KMC Complex.
Mchezo mwingine utapigwa mkoani Tanga wenyeji Coastal Union wakiikaribisha Singida BS katika mchezo utakaopigwa saa 12 jioni.




