Wakati watani zao Simba wakirejea jijini Dar es salaam jana baada ya kutwaa kombe la Muungano, kikosi cha Yanga kilisalia visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa ligi kuu utakaowakutanisha na Simba kwa mara ya pili katika kipindi cha siku tano.
Jumapili May 03 timu hizo zitachuana tena katika mchezo wa ligi kuu ambao matokeo yake huenda yakawa na maamuzi kwenye mbio za ubingwa msimu huu.
Yanga chini ya kocha Pedro Goncalves imepania kulipa kisasi dhidi ya kipigo kutoka kwa watani zao Simba na kumaliza mfululizo wa mechi 7 za bila ushindi kwa Simba.
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wanaendelea na maandalizi yao kuelekea mchezo huku akibainisha kuwa wachezaji wao wote wako katika hali nzuri, hakuna changamoto za majeruhi wapya baada ya fainali ya komb la Muungano.




