Simba yarejea Dar, mashabiki wamiminika kupokea taji

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th April 2026


Simba yarejea Dar, mashabiki wamiminika kupokea taji

Shangwe na nderemo zimetawala jijini Dar es Salaam kufuatia kurejea kwa mabingwa wapya wa Kombe la Muungano, Simba SC, waliowasili kutoka Zanzibar walikokwenda kuweka historia nyingine muhimu.

Simba walitwaa taji hilo baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye New Amaan Complex. Ushindi huo ulihitaji dakika 120 kuamuliwa.

Mara baada ya kuwasili bandarini, walipokelewa kwa shangwe kubwa na maelfu ya mashabiki wa Simba waliomiminika kusherehekea mafanikio hayo.

Huu ni ubingwa wa pili kwa Simba tangu mashindano ya Kombe la Muungano yaliporejeshwa rasmi mwaka 2024, ukiwa ni ubingwa wa 7 katika historia ya jumla ya mashindano hayo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.