Mabula kuibukia Ligi Kuu Uturuki

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th April 2026


Mabula kuibukia Ligi Kuu Uturuki

Kiungo wa Kitanzania, Alphonce Mabula anayekipiga Shamakhi FC nchini Azerbaijan, anatajwa kuwa kwenye rada za klabu ya Kasmpaa inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki.

Mabula, ambaye mkataba wake na Shamakhi unatarajiwa tamati Juni 30 mwaka huu, amekuwa muhimili mkubwa kwenye safu ya kiungo tangu ajiunge nayo akitokea FK Spartak Subotica ya Serbia.

Inaelezwa kuwa mabosi wa Kasimpasa wamevutiwa na nidhamu yake uwanjani, uwezo wa kukaba na kuanzisha mashambulizi. Tayari mazungumzo ya awali kati ya menejimenti ya mchezaji na klabu hiyo yameripotiwa kuanza.

Kama dili hilo litatiki, Mabula ataungana na mastaa wengine wa Kitanzania wanaokiwasha Uturuki kama Novatus Miroshi (Goztepe) na Diana Msewa (Trabzonspor)


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.