FIFA wabadilisha sheria za uwanjani kuelekea World cup 2026

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 29th April 2026


FIFA wabadilisha sheria za uwanjani kuelekea World cup 2026

Baraza la FIFA limepitisha mabadiliko muhimu ya sheria yatakayotumika katika FIFA World Cup 2026, yakilenga kubadilisha mwenendo wa mchezo na kuongeza nidhamu kwa wachezaji wote, kuanzia nyota wakubwa hadi wale wa benchi. Hatua hii inaashiria mwanzo wa enzi mpya ya usimamizi wa soka katika mashindano hayo yatakayofanyika katika United States, Canada na Mexico.

Miongoni mwa mabadiliko hayo, FIFA imeamua kufuta kadi zote za njano baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi, pamoja na kuzifuta tena baada ya robo fainali. Uamuzi huu unalenga kuwapa wachezaji nafasi ya kuanza upya katika hatua muhimu za mashindano, hivyo kupunguza uwezekano wa nyota wakubwa kukosa mechi za nusu fainali au fainali kutokana na mkusanyiko wa kadi za njano.

Aidha, FIFA imeimarisha adhabu kwa vitendo vinavyochukuliwa kama kukosa nidhamu uwanjani. Mchezaji atakayetoka uwanjani kwa hasira akipinga maamuzi ya mwamuzi ataonyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja. Vilevile, mchezaji atakayefunika mdomo wake wakati wa mabishano na mpinzani ataadhibiwa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, hatua inayolenga kuongeza uwazi na heshima ndani ya mchezo.

Kwa ujumla, mabadiliko haya yanakusudia kulinda heshima ya soka, kupunguza vitendo vya kupoteza muda, na kuhakikisha kuwa wachezaji bora wanashiriki katika hatua za mwisho za mashindano. FIFA imeweka wazi kuwa Kombe la Dunia 2026 litakuwa na sura mpya lenye nidhamu zaidi, ushindani mkubwa, na mvuto wa kipekee kwa mashabiki duniani kote.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.