Samatta anaendelea kutupia Ligi 1

Joel JJ By Joel JJ • 27th April 2026


Samatta anaendelea kutupia Ligi 1

Nahodha wa timu ya Taifa Ya Tanzania, Mbwana Samatta, ameendelea kung’ara katika ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) baada ya kufunga tena katika mchezo uliopigwa Jumapili, Aprili 26, 2026.

Samatta, anayekipiga katika klabu ya Le Havre AC, alifunga bao la mapema katika dakika za mwanzo za mchezo dhidi ya FC Metz mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 4-4.

Bao hilo linaongeza mchango wake muhimu katika kikosi cha Le Havre ambacho kinaendelea kupambana katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

Huu ni muendelezo wa kiwango kizuri kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu mbalimbali barani Ulaya, ambaye sasa anaonekana kuzoea mazingira ya Ligue 1 na kurejea katika ubora wake.

Mbali na kufunga, Samatta ameendelea kuwa kiungo muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu yake kwa kutumia uzoefu wake mkubwa katika soka la kimataifa.

Kiwango chake kinatoa matumaini makubwa kwa Tanzania kuelekea michuano ya Afcon 2027, itakayofanyika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.