Ibenge aipania Yanga nusu fainali Muungano Cup

Joel JJ By Joel JJ • 24th April 2026


Ibenge aipania Yanga nusu fainali Muungano Cup

Kocha Mkuu wa Azam Fc Florent Ibenge amesema kikosi chake kitakuwa tayari kwa mchezo wa nusu fainali kombe la Muungano dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa New Amaan Complex.

Azam Fc walitinga nusu fanali ya michuano hiyo baada ya kuichapa KVZ mabao 2-0 huku Yanga ambao ni mabingwa watetezi, wakiichapa Muembe Makumbi mabao 4-0 kwenye mchezo wa robo fainali.

Ibenge ametamba kuwa kikosi chake kitakuwa tayari kukabiliana na timu bora zaidi Tanzania Bara (Yanga) wakitoka kuiondosha mashindanoni timu bora visiwani Zanzibar (KVZ)

“Ni kweli tunakwenda kukutana na Yanga, utakuwa mchezo mgumu lakini sisi Azam hizo ndio mechi ambazo wakati wote tunapenda kuzicheza, tutajiandaa sawasawa kukutana nao"

“Mechi za namna hii zinakuimarisha na kujua ubora wa timu yako, tumetoka kuitoa timu bora ya hapa Zanzibar, haikuwa rahisi lakini tutakwenda kukutana tena na timu bora ya Ligi ya Bara,” alisema.

Hii itakuwa mechi ya tatu kwa Azam Fc kukutana na Yanga mwaka huu ikiwa ni ya pili timu hizo kukutana visiwani Zanzibar.

Yanga ilitwaa taji la Mapinduzi mwezi Januari baada ya kuifunga Azam Fc kwa mikwaju ya penati baada ya suluhu ya bila kufungana.

Timu hizo pia zimekutana kwenye mchezo wa ligi kuu ambao pia ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.