Mlandege Fc imeiduwaza Singida BS leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali kombe la Muungano.
Baada ya Muembe Makumbi na kVZ kutupwa nje kwenye michuano hiyo jana, Mlandege Fc imekuwa timu ya kwanza ya visiwani Zanzibar kutinga nusu fainali sasa ikisubiri mshindi wa mchezo kati ya Mfunzo dhidi ya Simba.
Singida BS wanarejea Bara kujiandaa na mechi za ligi kuu na kombe la CRDB





