Dirisha la usajili linazidi kukaribia na vilabu vikubwa barani Ulaya vinaendelea kupanga mikakati ya kuimarisha vikosi vyao. Hizi hapa ni tetesi kuu za leo kutoka vyanzo mbalimbali vya michezo:
Arsenal na Barcelona Wamuwania Bernardo Silva
Kwa mujibu wa ESPN Brazil, Arsenal FC na FC Barcelona zinaangalia uwezekano wa kumsajili Bernardo Silva iwapo ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu.
Liverpool na Juventus Wamuwania Kolo Muani
Ripoti kutoka Gazzetta dello Sport zinaeleza kuwa Liverpool FC wanamtaka Randal Kolo Muani wa Paris Saint-Germain kama mbadala wa Mohamed Salah, huku Juventus FC nao wakimuwania.
Manchester United Wawinda Viungo Wapya
Kwa mujibu wa The Telegraph, Manchester United wanawafuatilia Elliot Anderson wa Nottingham Forest na Aurelien Tchouameni wa Real Madrid kama mbadala wa Casemiro.
Brighton Wamtaka James Trafford
Ripoti kutoka Florian Plettenberg zinaonyesha kuwa Brighton & Hove Albion wanaweza kumsajili James Trafford kutoka Manchester City.
Mainoo Kukaa Manchester United
Kwa mujibu wa The Sun, Kobbie Mainoo amekubali kufanya mazungumzo ya mkataba mpya wa miaka mitano na Manchester United.
Koopmeiners Awaniwa na United na Galatasaray
Ripoti za Tuttosport zinaeleza kuwa Manchester United na Galatasaray wanamuwania Teun Koopmeiners wa Juventus FC.
Barcelona Waongoza Mbio za Eduardo Conceicao
Kwa mujibu wa Teamtalk, FC Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili Eduardo Conceicao wa Palmeiras, huku Manchester City, Manchester United na Newcastle United nazo zikivutiwa.
West Ham Wapanga Kumuza Mavropanos
Kwa mujibu wa Football Insider, West Ham United wako tayari kumuuza Konstantinos Mavropanos huku vilabu vya Bundesliga vikimuwania.
Chelsea na United Wamfuatilia Alex Scott
Ripoti kutoka CaughtOffside zinaeleza kuwa Chelsea FC na Manchester United wanamfuatilia Alex Scott wa AFC Bournemouth.
Leeds United Wamtunza Ethan Ampadu
Kwa mujibu wa Teamtalk, Leeds United wanapanga kumpa mkataba mpya Ethan Ampadu.



