Real Madrid kumaliza hasira kwa Alaves leo?

Joel JJ By Joel JJ • 21st April 2026


Real Madrid kumaliza hasira kwa Alaves leo?

Real Madrid inatarajiwa kushuka dimbani leo Jumanne, Aprili 21, 2026, kuikaribisha Deportivo Alavés katika mwendelezo wa michezo ya La Liga

Mchezo huo utapigwa katika dimba la Santiago Bernabéu Stadium saa 4:30 usiku, ukiwa sehemu ya ratiba ya raundi ya 33 ya ligi hiyo.

Real Madrid wanaingia katika pambano hilo wakisaka ushindi muhimu ili kuendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa wa La Liga wakati Alavés wakihitaji pointi ili kujinusuru na hatari ya kushuka daraja.

Kocha wa Madrid Alvaro Arbeloa anatarajiwa kuwategemea nyota wake muhimu akiwemo Jude Bellingham, Vinícius Júnior na Kylian Mbappe kumpatia ushindi ili kupunguza presha inayoweka matatani hatma yake ya kuendelea kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria barani Ulaya.

Hizi hapa ni mechi zinazopigwa leo:

  • Athletic Club vs CA Osasuna — saa 20:00
  • RCD Mallorca vs Valencia CF — saa 20:00
  • Girona FC vs Real Betis — saa 22:30

  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.