Kikosi cha Azam Fc kimewasili Visiwani Zanzibar leo tayari kushiriki michuano ya kombe la Muungano inayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia kesho Jumanne, April 21 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Azam Fc watashuka dimbani siku ya Jumatano kuikabili KVZ katika mchezo wa robo fainali.
Wauza ice cream hao wanaweza kukutana na Yanga katika hatua ya nusu fainali kama watashinda mchezo dhidi ya KVA huku Wananchi nao wakishinda mchezo dhidi ya Muembe Makumbi utakaopigwa kesho Jumanne.








