Kikosi cha Yanga kimewasili Visiwani Zanzibar leo tayari kushiriki michuano ya kombe la Muungano inayotarajiwa kuanza kesho Jumanne, April 21 katika uwanja wa New Amaan Compex.
Yanga itafungua pazia ya michuano hiyo hapo kesho kwa mchezo dhidi ya Muembe Makumbi utakaopigwa saa 1 usiku dimba la Amaan.
Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo wakitwaa yaji msimu uliopita ikiwa huu ni msimu wa tatu tangu michuano hiyo iliporejeshwa rasmi.
Msimu wa kwanza Simba waliibuka mabingwa, msimu huu klabu nane zikichuana kuwania taji hilo.
Bingwa wa michuano hiyo mwaka huu ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 150, ikiwa ni ongezeko la mara tatu zaidi ya zawadi ya mwaka jana (Milioni 50). Mshindi wa pili atajinyakulia Shilingi Milioni 100.
Klabu za Yanga, Simba, Azam Fc na Singida BS zitashiriki michuano hiyo zikiwakilisha Tanzania bara wakati KVZ, Mlandege, Mafunzo na Muembe Makumbi zikiwakilisha upande wa Zanzibar



