Fei Toto namba zake zinazungumza Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th April 2026


Fei Toto namba zake zinazungumza Ligi Kuu

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum maarufu kama 'Fei Toto', ameendelea kuwa nguzo muhimu ya timu hiyo akionyesha kiwango cha juu katika Ligi Kuu Bara.

Ijumaa usiku, Fei Toto aliiongoza Azam Fc kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa ligi kuu ya NBC akitoa asisti 2

Msimu huu wa 2025/26, Fei Toto ameshiriki moja kwa moja katika mabao 14 mpaka sasa, akifunga mabao 7 na kutoa assisti 7.

Fei Toto amekuwa na mwendelezo mzuri katika misimu mitatu aliyoitumikia Azam Fc.

Msimu wa 2024/25, Fei Toto aliongoza kwa assisti katika Ligi Kuu Bara baada ya kuisaidia Azam FC kufanikisha mabao 17 (mabao manne na assisti 13).

Aidha, mwaka 2024 ulikuwa wa dhahabu kwa nyota huyu, baada ya kuisaidia timu yake kufanikisha mabao 27 (mabao 15 na assisti 12), akimzidi Stephane Aziz Ki wa Yanga aliyefanikisha mabao 21 (mabao 12 na assisti tisa).

Msimu wa 2023/24, Fei Toto alifunga mabao 19 ya Ligi Kuu Bara, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji miongoni mwa wachezaji, nyuma ya Aziz Ki aliyefunga 21. Pia, alijitokeza katika Kombe la Shirikisho (FA), akiisaidia Azam FC kufika fainali kwenye New Amaan Complex Juni 2, 2024, ambapo walipoteza kwa penalti 6-5 dhidi ya Yanga baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120.

Kwa misimu mitatu mfululizo, Fei Toto ameonyesha kuwa si tu mchezaji mwenye ubora wa kipekee, bali pia ni kiungo muhimu katika kikosi cha Azam FC.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.