Soko la usajili linaendelea kupamba moto barani Ulaya huku klabu zikianza kuweka wazi malengo yao ya majira ya kiangazi. Hizi hapa ni tetesi kuu za leo kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika:
Liverpool Wamkaribia Marcos Senesi
Kwa mujibu wa i, Liverpool FC wanaongoza katika mbio za kumsajili Marcos Senesi wa AFC Bournemouth, ambaye mkataba wake unakaribia kuisha.
City na Bayern Wamtaka Givairo Read
Ripoti kutoka Sky Sports zinaeleza kuwa Manchester City wanamfuatilia Givairo Read wa Feyenoord, huku Bayern Munich nao wakionyesha nia.
Liverpool Wawania Gordon na Ndiaye
Kwa mujibu wa Teamtalk, Liverpool FC wanavutiwa na Anthony Gordon wa Newcastle United pamoja na Iliman Ndiaye wa Everton FC ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Mourinho Aweza Kutua Newcastle
Ripoti za talkSPORT zinaeleza kuwa Jose Mourinho anaweza kuwa chaguo la Newcastle United iwapo watamua kumtimua Eddie Howe.
Bournemouth Wakaribia Kumnasa Marco Rose
Kwa mujibu wa The Telegraph, AFC Bournemouth wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumteua Marco Rose kuwa kocha wao mpya.
Vita ya Coulibaly Yazidi Kupamba Moto
Gazeti la Bild linaripoti kuwa Chelsea FC na Newcastle United zinachuana kumsajili Karim Coulibaly wa Werder Bremen.
Juventus Wawatazama Alisson na Bernardo Silva
Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, Juventus FC wanawafuatilia Alisson Becker wa Liverpool FC na Bernardo Silva wa Manchester City.
Newcastle Wamrudia Diomande
Football Insider linaeleza kuwa Newcastle United wako tayari kurejea tena kwa Ousmane Diomande wa Sporting CP, ambaye thamani yake ni zaidi ya pauni milioni 40.
Jacobo Ramon Awaniwa na Vigogo
Kwa mujibu wa Teamtalk, Jacobo Ramon wa Como 1907 anawindwa na Arsenal FC na Chelsea FC.
Arsenal Yapanga Kumnasa Julian Alvarez
Ripoti kutoka CaughtOffside zinaeleza kuwa Arsenal FC wako tayari kuwauza Gabriel Jesus na Kai Havertz ili kupata fedha za kumsajili Julian Alvarez wa Atletico Madrid.



