Yamal na ujumbe kwa mashabiki wa Barca

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media • 15th April 2026


Yamal na ujumbe kwa mashabiki wa Barca

Nyota chipukizi wa FC Barcelona, Lamine Yamal, ametuma ujumbe mzito na wa kihisia kwa mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kuondolewa kwenye UEFA Champions League.

Katika ujumbe wake, Yamal alieleza maumivu makubwa aliyoyapata baada ya ndoto ya kutwaa taji hilo kufifia:

“Kwa kweli sina maneno ya kuelezea ninavyohisi kwa sasa. Nimekaa gizani, bado siamini kwamba imeisha. Kwa mashabiki wetu — naomba radhi sana. Tumewaangusha tena, na huu ni uchungu nitakaoubeba kila usiku hadi tutakapolirekebisha hili. Mnatusafiria, mnashangilia, mnalia kwa ajili yetu, lakini usiku huu tumewapa maumivu zaidi tu.”

Yamal aliweka wazi kuwa ndoto yake kubwa tangu alipojiunga na akademi ya La Masia ni kuirejesha Barcelona kileleni mwa Ulaya, na kushindwa kufanikisha hilo kwa sasa kunamuumiza sana:

“Nimekuwa nikiota kuirudisha nyumbani hii kombe tangu siku yangu ya kwanza La Masia. Ni kitu pekee ninachotaka. Kuiona ikitupita hivi ni kama ndoto mbaya ambayo siwezi kuamka.”

Hata hivyo, kijana huyo mwenye umri mdogo aliahidi kutokata tamaa, akisisitiza kuwa ataendelea kupambana hadi kufanikisha ndoto hiyo:

“Nisikilize sasa: sitaacha kamwe. Haijalishi itachukua miaka mingapi au nitahitaji kujitoa kiasi gani — sitapumzika hadi kombe hilo lirudi Barcelona mahali linapostahili. Maisha yangu, roho yangu na kila jasho langu ni kwa ajili ya klabu hii. Tutarudi tena. Na nawaahidi hilo.”


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.