PSG yatinga nusu fainali, Safari ya Liverpool yafika tamati kwa rekodi mbaya uefa

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media • 15th April 2026


PSG yatinga nusu fainali, Safari ya Liverpool yafika tamati kwa rekodi mbaya uefa

Klabu ya Paris Saint-Germain imeandika historia mpya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield, na kufuzu hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League kwa ubora mkubwa.

Mchezo huo ulikuwa wa kipekee kwa PSG, ambao waliidhibiti Liverpool katika mechi zote mbili za robo fainali bila kuruhusu bao lolote , jambo ambalo halijawahi kutokea dhidi ya Liverpool katika historia ya kisasa ya mashindano hayo. Shujaa wa usiku huo alikuwa Ousmane Dembélé, aliyefunga mabao yote mawili na kuiongoza PSG kwa ushindi muhimu ugenini.

Kwa ushindi huo, PSG wamefikisha mechi tisa mfululizo bila kupoteza katika hatua za mtoano za Champions League, rekodi mpya inayothibitisha ubora wao katika mashindano hayo msimu huu.

Kwa upande wa Liverpool, hii ni historia ya kusikitisha kwani kwa mara ya kwanza wanashindwa kufunga bao katika michezo miwili mfululizo ya hatua za mtoano, licha ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani unaotambulika kwa presha kubwa kwa wapinzani.

Kocha Arne Slot alijaribu kufanya mabadiliko mbalimbali ya kiufundi, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda huku PSG wakionekana kuwa bora katika kila idara ya mchezo.

Kwa sasa, PSG wanaungana na Atlético Madrid katika hatua ya nusu fainali, wakiwa na dhamira moja kuu ya kupigania taji la Champions League na kuthibitisha ubora wao barani Ulaya.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.