Arsenal wapoteza tena EPL, Bournemouth wawanyanyasa Emirates

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th April 2026


Arsenal wapoteza tena EPL, Bournemouth wawanyanyasa Emirates

Klabu ya Arsenal imeendelea kuporomoka kwenye mbio za ubingwa wa Premier League baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa AFC Bournemouth katika mchezo uliochezwa leo Jumamosi, Aprili 11, 2026.

Katika mchezo huo uliopigwa dimbani Emirates, Bournemouth waliandika historia kwa ushindi muhimu uliotikisa mbio za ubingwa. Wageni hao walitangulia kufunga kupitia chipukizi Eli Junior Kroupi kabla ya Arsenal kusawazisha kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Viktor Gyokeres.

Hata hivyo, bao la ushindi lilipatikana dakika ya 74 kupitia Alex Scott, aliyewanyamazisha mashabiki wa nyumbani na kuipa Bournemouth alama tatu muhimu.

Matokeo hayo ni pigo kubwa kwa kikosi cha kocha Mikel Arteta, huku yakizidi kuibua maswali kuhusu uwezo wao wa kuhimili presha ya mbio za ubingwa, hasa baada ya kupoteza michezo kadhaa ya hivi karibuni.

Matokeo Mengine ya EPL Leo (Aprili 11, 2026)

Mbali na mchezo huo wa Arsenal, michezo mingine ya ligi hiyo ilichezwa na kutoa matokeo yafuatayo:

  • Brentford 2-2 Everton
  • Burnley 0-2 Brighton & Hove Albion

Matokeo haya yanaendelea kufanya mbio za ubingwa na nafasi za juu kuwa ngumu zaidi, huku timu mbalimbali zikionyesha ushindani mkali kuelekea mwisho wa msimu.

Kwa sasa, Arsenal wanahitaji kurejea kwenye kiwango chao cha awali haraka ili kuendelea kubaki kwenye nafasi nzuri ya kuwania taji hilo, vinginevyo wapinzani wao Man City wanaweza kutumia mwanya huo kuwafikia.

Kama Man City watashinda mechi mbili za viporo, watafikisha alama 67 na kuwa tofauti ya alama tatu dhidi ya vinara hao wa Premi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.