Benchi Azam Fc lamchosha Fofana

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th April 2026


Benchi Azam Fc lamchosha Fofana

Kipa raia wa Ivory Coast, Issa Fofana, anaonekana kuwa kwenye wakati mgumu ndani ya kikosi cha Azam FC, hali iliyozua tetesi kuwa anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa za karibuni, Fofana anafikiria kurejea kwa waajiri wake wa zamani, Al Hilal Omdurman, baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Fofana alisajiliwa na Azam FC akiwa na matarajio ya kuwa kipa namba moja, lakini hali imekuwa tofauti baada ya kuongezeka kwa ushindani mkali ndani ya timu.

Kipa Aishi Manula amerejea kwenye kiwango bora, akihusishwa na takwimu nzuri za clean sheets saba katika mechi nane, hali iliyomfanya kuimarisha nafasi yake kikosini.

Pia, chipukizi Zuber Foba ameendelea kuonyesha uwezo wake, na kuongeza ushindani katika nafasi ya ulinzi wa lango.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mchezaji huyo, Al Hilal Omdurman wanafuatilia kwa karibu hali ya Fofana na wanaweza kuchukua hatua ya kumrudisha endapo Azam FC wataamua kumtoa katika dirisha lijalo la usajili.

Fofana aliwahi kufanya vizuri akiwa Sudan wakati Al Hilal ikiwa chini ya kocha Florent Ibenge ambaye ndiye aliyependekeza usajili wake kujiunga na Azam Fc lakini amekabiliwa ushindani mkali kutoka kwa walinda lango wa ndani.

Bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Azam FC kuhusu mustakabali wa kipa huyo, lakini dalili zinaonyesha kuwa kwenye usajili wa dirisha lijalo huenda wakamruhusu mlinda lango huyo kusaka changamoto sehemu nyingine.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.