Minziro atajwa KMC

Joel JJ By Joel JJ • 9th April 2026


Minziro atajwa KMC

Klabu ya KMC hivi karibuni ilitangaza kuachana na kocha mkuu Abdallah Mohamed “Bares” pamoja na benchi lote la ufundi kufuatia matokeo duni yanayowakabili msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hatua hii imekuja baada ya timu kushika nafasi za chini kwenye jedwali, jambo lililosababisha uongozi kufanya maamuzi hayo ili kuinusuru klabu hiyo na janga la kushuka daraja.

Kwa sasa, uongozi wa KMC unatafuta kocha mpya atakayechukua nafasi ya benchi la ufundi na kujaribu kubadilisha mwenendo wa timu.

Miongoni mwa majina yanayotajwa ni Fred Felix Minziro maarufu kama “Majeshi”, kocha mwenye uzoefu mkubwa nchini Tanzania. Minziro anatajwa kuwa miongoni mwa wale wanaoweza kuvaa viatu vilivyowashinda makocha waliotangulia, Marcio Maximo na Mohamed Bares.

Minziro anatambulika miongoni mwa makocha wenye mbinu na uwezo wa kuinua kikosi chenye changamoto kubwa, pia akisifika kwa kuzipandisha daraja timu mbalimbali kutoka madaraja ya chini.

KMC wamekusanya alama nane tu msimu katika mechi 18 ni wazi dalili za kuelekea championship zinaonekana na pengine kazi ya ziada inapaswa kufanyika kuwanusuru na janga la kushuka daraja.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.