Wiki mpya imeanza kwa moto katika soka la Ulaya, huku majina makubwa yakihusishwa na uhamisho unaoweza kubadilisha kabisa taswira ya vilabu vikubwa. Hizi hapa ni tetesi zinazoongoza leo:
Vinicius Jr Aingia Sokoni?
Vilabu vya Manchester United, Manchester City, Chelsea na Arsenal vimejulishwa kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa Vinicius Junior kutoka Real Madrid (TeamTalk).
Ugarte Huenda Akaondoka United
Manuel Ugarte anaweza kuuzwa na Manchester United, huku Newcastle United, Aston Villa na Juventus zikimtaka (CaughtOffside).
Liverpool Wapanga Dili la Kubadilishana
Liverpool wanafikiria kumtoa Mohamed Salah na kumchukua Marcus Leonardo wa Al Hilal katika dili la kubadilishana wachezaji (GiveMeSport).
Amadou Onana Awindwa na United
Amadou Onana wa Aston Villa anaweza kuondoka kwa dau kubwa, huku Manchester United wakimtaka (Football Insider).
Vuskovic Afunguka Kuhusu Hatma Yake
Luka Vuskovic wa Tottenham Hotspur, anayekipiga kwa mkopo Hamburger SV, amesema anaweza kurejea klabuni licha ya kuvutiwa na timu kubwa (Evening Standard).
Chelsea Wamtazama Kipa Mpya
Chelsea wanapanga kumsajili Robin Roefs wa Sunderland kama mbadala wa Robert Sanchez (TeamTalk).
Leverkusen Wapanga Kumbakiza Diomande
Bayer Leverkusen wanataka kuongeza mkataba wa Yan Diomande kwa mwaka mmoja zaidi licha ya kuvutiwa na vilabu vikubwa (Fabrizio Romano).



